Wanasiasa wapigwa marufuku kuwa Viongozi ndani ya ushirika Mrajisi


Na Timothy Itembe Mara.

Kaimu mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Mara, Kija Maheda amewapiga marufuku wanasiasa walio na mawazo ya kuwa viongozi ndani ya Ushirika na kuwa kufanya hivyo nikosa la kisheria.

Maheda alisema jana katika mkutano wa WAMACU  kuwa sheria iko wazi ya vyama vya ushirika inakataza wanasiasa kuwa viongozi ndani ya ushirika na kuwa kufanya hivyo nikosa la jinai.

“Kifungu 132 namba 1,2,3,na 4 ya sheria ya vyama vya ushirika namba 06 ya mwaka 2013 inakataza wanasiasa kuwa viongozi ndani ya vyama vya ushirika na kuwa kufanya hivyo nikosa la kisheria”alisema Maheda. 

Kifungu hicho kinawataja wazi viongozi wa siasa ambao hawaruhusiwi kuwa viongozi ndani ya vyama vya ushirika kuwa ni pamoja na mwenyekiti yeyote ambaye anapatikana kupitia siasa kama vile mwenyekiti wa kijiji,mwanakamati/Mjumbe wa kijiji,Diwani na Mbunge.

Wengine ni  Mtendaji wa mtaa/Kijiji,Mtendaji Kata,Mkuu wa wilaya mkuu wa mkoa na kuwa viongozi hao wote hawaruhusiwi kuingilia maswala ya ushirika kwani kufanya hivyo wataingiza siasa katika usgirika.

Katika kikao hicho wajumbe alipitisha taarifa na Bajeti ya hali ya ukusanyaji na uuzwaji wa kahawa msimu wa mwaka 2018/2019 pamoja na mapato na matumizi makao makuu kwa msimu 2019/2020.

Kwa upande wake Meneja WAMACU,Jeremiah Mugendi alisema kuwa taarifa ya ukusanyaji wa kahawa  2018/2019 katika Gala la WAMACU Limeted hadi kufikia 30,03,2019 jumla ya tani 220,260 mzimepokelewa kati ya hizo zilizokobolewa na kuuzwa ni tani,209,160 kahawa ambayo haujauzwa ni kg 11,100 ikiwa ni madaraja mbalimbali.

Lukas Massa ambaye ni mratibu wa shugili za WAMACU,alisema kuwa WAMACU ni wasimamizi na waratibu wa shuguli za ukusanyaji na kuhifadhi kahawa kwa mfumo wa stakabadhi Galani.

Massa alifafanua kuwa msimu wa 2018/2019 wakulima wa Mara Coopertive Union Limeted walikusanya Kg 451386 kutoka kwa wanachama wake(Vyama vya msingi) kwaajili ya kuhifadhi,kukoboa na kuitafutia soko na kuwa kahawa safi kg 451,382 zilizokusanywa zilikobolewa zote hadi Februal 28,2019 kahawa safi zilizopatikana kg 220,260 zilizouzwa mnadani kg 209,160 na kubaki kahawa safi ambayo haijauzwa kg 11,1000 kahawa kg 209,160 ziliuzwa USD 252,884.60 sawa na shilingi 583,109,249 hadi sasa hakuna wakulima wanaodai.