Na. John Walter-Manyara
Mtu mmoja amefariki papo hapo dunia na wanne kujeruhiwa baada ya gari la abiria kugongana uso kwa uso na gari dogo lililokuwa limebeba wanafunzi wa shule ya msingi.
Akiwa katika eneo la tukio Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:30 asubuhi leo May 14.2019 ikihusisha gari la abiria kampuni ya Mtei inayofanya safari zake Babati-Dar es salaam lenye namba za usajili T 299 AXP Scania Marcopolo ikiendeshwa na Japhet Limo (35) mkazi wa Babati kuligonga gari dogo Hiace lenye namba T 590 BHZ Nissan Carravan iliyokuwa ikiendeshwa na Daniel Godfrey (25) mkazi wa Bonga iliyokuwa imebeba wanafunzi na walimu wa shule ya Silver Leaf English Medium ikitokea Bonga kuelekea shuleni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga ambaye alifika eneo la tukio amemtaja aliepoteza Maisha ni mwanafunzi wa shule ya English Medium Pre-Primary iliyokuwa ikijukiana kwa jina la Debora na sasa Silver Leaf Academy aliefahamika kwa jina la Osiligi Emmanuel mwenye umri wa miaka 3.5 [miaka mitatu na nusu] huku mwingine ambaye nae ni mwanafunzi wa shule hiyo Lightnes Emmanuel Daudi (6) mkazi wa Bonga akiwa mahututi.
Waliojeruhiwa ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mrara ni, dereva wa Hiace Daniel Godfrey (25) ,Francis Mollel mwalimu wa shule ya Silver Leaf Academy (39).
Kwa mujibu wa mashuhuda ”dereva wa gari hiyo ya abiria alipofika Himiti Babati mjini akiwa katika mwendo kasi alitaka kuipita gari iliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari ndipo ilipokutana uso kwa uso na kupelekea kifo cha mwanafunzi mmoja papo hapo.
Kamanda mesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari la upande wa kushoto bila kuchukua tahadhari.
Hata hivyo Dereva huyo baada ya ajali hiyo alikimbia pasipo julikana na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta ili afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.