Agizo la Waziri Jaffo lawaamsha usingizini Viongozi Arusha


Serikali ya wilaya ya Arusha kwa kushirikiana na jiji la Arusha imeanza kutekeleza agizo la waziri wa nchi ofisi ya Rais, TAMISEMI,Suleiman Jaffo alilotaka  jengo la hospitali mpya ya Wilaya ambalo ujenzi wake umekamikija  kuanza kutoa Huduma Mara Moja  kwa wananchi.

Mei 25, mwaka huu Waziri Jaffo alitembelea mradi wa jengo hilo uliopo eneo la Njiro Kontena jijini hapa na kukuta limekamilika muda mrefu lakini halifanyi Kazi ,ambapo alitoa wiki mbili kwa uongozi wa wilaya na halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha hospital hiyo inafunguliwa Mara Moja na kutoa Huduma kwa wananchi.

Akiongea na vyombo vya habari katika hospital hiyo Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqqar alisema hospitali hiyo tayari imeshaanza kutoa Huduma za chanjo na inatarajiwa kuanza kutoa Huduma zingine za matibabu muda mfupi ujao baada ya vifaa Tiba kuwasili.

Katika hatua nyingine  Dagarro alisema wilaya hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Arusha ,imeingia mkataba wa ujenzi wa jengo lingine la Mama na Mtoto linalojengwa katika hospitali hiyo na kampuni ya ukandarasi ya BQ Contractors LTD ya jijini Dar as salaam.

Alisema mradi huo utagharimu kiasi cha sh. Bilioni 1.36 fedha ambazo ni za ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha na utakamilika katika kipindi cha miezi saba kuanzia sasa.

“Leo tumekuja kumkabidhi ukandarasi ujenzi wa jengo la Matenet ambalo utenzi wake utachukua miezi saba kukamikika,” alisema Daqqar.

Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya BQ, Mhandisi John Bura alisema kuwa katika kipindi cha miezi saba ya Mkataba  watahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati katika kiwango kinachotakiwa.

“Tutahakikisha tunatekeleza mradi huu kwa viwango vya hali ya juu katika muda tuliokubaliana, "alisema Mhandisi Bura.

Awali Mkurugenzi wa jjji la Arusha,Dkt Maulid Madeni alisema  kuwa kuchelewa kufunguliwa kwa hospital ya wilaya ambayo ujenzi wake umekamilika kumetokana na kubadilika kwa matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kiasi cha sh,milioni 100.