https://monetag.com/?ref_id=TTIb Bashungwa, Kichere kuapishwa leo | Muungwana BLOG

Bashungwa, Kichere kuapishwa leo


Rais Dk. John Magufuli leo anatarajiwa kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Charles Kichere, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inatokana na mabadiliko madogo ya mawaziri ambapo alitengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kumteua Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Pia Rais Magufulu alitengua uteuzi wa Kichere aliyekuwa Kamishna Mamlaka ya Mapato (TRA), ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe.