Loading...

6/14/2019

BET kutoa Tuzo ya heshima kwa marehemu Nipsey Hussle

Kwenye ugawaji wa tuzo za BET zitakazofanyika June 23,2019 Marehemu Nipsey Hussle atakabidhiwa tuzo ya heshima kutokana na alama ya maisha aliyoacha, Nipsey alifariki March 31,2019 baada ya kupigwa risasi nje ya duka lake ‘The Marathon Clothing” mjini Los Angeles.

Imeelezwa kuwa kutokana na mchango mkubwa aliouonyesha kwenye jamii Marehemu Nipsey Hussle enzi za uhai wake anastahili kutunukiwa tuzo ya utu (Humanitarian Award) kwa mengi aliyoyafanya kwenye ujasiriamali pamoja na muziki.

Inaripotiwa kuwa DJ Khaled, YG na John Legend watatumbuiza pamoja katika ugawaji wa tuzo na katika kumuenzi Nipsey Hussle kwa yale yote aliyoyafanya kwa jamii.
Loading...