Loading...

6/14/2019

Iran yakana kuhusika na milipuko ya meli

Jeshi la Marekani limetoa mkanda wa video unaoonyesha wanaoaminika kuwa wanajeshi wa kikosi cha wanamapinduzi wa Iran wakiondoa bomu ambalo bado lilikuwa halijalipuka kutoka kwenye meli moja ya mafuta kati ya meli mbili zilizolengwa na mashambulizi kwenye mlango wa bahari wa Hormuz katika Ghuba ya Oman.

Iran leo imekana na kusema kuwa jukumu lake ni kusimamia ulinzi wa Mlango wa Bahari wa Hormuz unaounganisha Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Oman, na kwamba kuilaumu Iran kwa mashambulizi ya meli za mafuta katika Ghuba ya Oman ni jambo la kushangaza.

 Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema usalama wa dunia nzima, hasa Ghuba ya Uajenmi ni muhimu sana kwa Iran.

Marekani hapo jana iliishutumu Iran kwa mashambulizi ya meli mbili za mafuta katika Ghuba hiyo ya Oman, hatua iliyopelekea kupanda kwa bei za mafuta na kuzua wasiwasi kuhusu mapambano mapya kati ya Marekani na Iran.
Loading...