Loading...

6/13/2019

Israel: Mke wa Waziri Mkuu atozwa faini ya Tsh. Milioni 35, kisa?


Mke wa Waziri Mkuu wa Israel, Sara Netanyahu, amekubali kulipa faini ya Shekeli Elfu 55 ambazo ni sawa na Tsh. Milioni 35 baada ya kukiri kosa la kuagiza chakula ndani ya makazi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, kesi hiyo imehusisha uagizwaji wa chakula chenye thamani ya Shekeli 175,000 sawa na Milioni 114 fedha za Kitanzania.

Kwa mujibu wa sheria za Israel, kuagiza huko chakula kulikofanywa na yeye binafsi ni kosa kisheria kwakua serikali ilikua imeweka mpishi maalum kwaajili ya makazi ya Waziri Mkuu,Familia na Wageni wake.

Imebanika kwamba Mke huyo wa Netanyahu alitumia fedha za Umma kuwalipa watu aliowaita kama "Vibarua" akificha ukweli kwamba watu hao walikua wahudumu kwenye dhifa mbalimbali za kitaifa
Loading...