Loading...

6/13/2019

Taifa Stars kuvaana na Misri leo


Nahodha wa Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, na Nyota wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta, Captain Diego, leo ataiongoza timu hiyo kucheza mechi ya kirafiki na Misri 'Pharao'.

Mchezo huo ambao utachezwa Uwanja wa Borg El Arab, kuanzia Saa 4:00 Usiku, Misri itaongozwa na Mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mwamba wa Liverpool, Mfalme wa Misri, Ustaadh, Mohamed Salah.

Dimba la Borg El Arab, sio geni kwa baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars hasa kwa wale wanaotoka Yanga SC kama Kelvin Yondani na wale wa Simba SC kama Erasto Nyoni na John Bocco, kwani kwa nyakati tofauti wakichezea timu zao.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger