Loading...

Jun 13, 2019

Rais Magufuli akerwa na wizara, Tanesco kutowajibika


Rais John Magufuli awakanya viongozi wa Wizara ya Nishati na Tanesco kwa kushindwa kuwasaidia wabunifu wa kufua umeme kutoka Njombe, Jairos Ngailo na John Mwafute maarufu kama Pwagu.

Akizungumza leo  katika mkutano na wabunifu hao wa mitambo midogo ya kufua umeme uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,

Rais amesema licha ya wataalamu hao kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu, hakuna yeyote aliyejitokeza kuwasaidia.

“Wangekuwa wameshasaidiwa wasingefika hapa. Transfoma zingekuwepo, mkurugenzi wa Tanesco kwao ni Njombe na nina uhakika huwa anaenda likizo huko lakini hajafanya lolote. Meneja wa Tanesco mkoa (Njombe) nimemsikia akizungumza hawa waje wanione  kisha waende Ewura Yeye hakutaka shida."

“Hata wangezalisha umeme ukaleta madhara shida isingekuwa kwa watendaji wa Tanesco, kwa hiyo Mkurugenzi wa Njombe naye hajaleta taarifa yoyote kuhusiana na wagunduzi hawa tangu mwaka 1980.”

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger