Mwandishi habari Urusi aanguka kituo cha polisi


Mwanasheria wa mwandishi wa habari wa Urusi Ivan Golunov, anayeshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya, amesema mteja wake alianguka siku ya Jumamosi na kupelekwa hospitali.

Amesema, Golunov alianguka akiwa katika kituo cha polisi, muda mfupi kabla ya kusikilizwa kwa kesi ya dawa za kulevya inayomkabili. Mwandishi huyo, alikamatwa mjini Moscow akielekea kukutana na mtoa habari wake wakati polisi walipogundua dawa za kulevya katika mkoba nyumbani kwake.

Chombo cha habari cha Meduza anakofanya kazi mwandishi huyo, pamoja na vyombo vingine huru vya habari, vimekuwa vikidai kuwa, polisi walipandikiza dawa za kulevya nyumbani kwa mwandishi huyo, ambaye hutoa habari za kiuchunguzi kuhusu rushwa pamoja na shughuli zisizo halali mjini Moscow.