Rais Donald Trump wa Marekani amesema jana kuwa atakuwa tayari kupokea taarifa kutoka nchi ya kigeni kuhusiana na mpinzani wake katika uchaguzi wa mwaka 2020, baada ya miaka kadhaa ya kukana kwamba Urusi ilimsaidia kushinda uchaguzi.
Mahusiano ya timu ya Trump na Urusi wakati wa uchaguzi wa rais mwaka 2016 yamesababisha uchunguzi uliofanywa na mchunguzi maalum Robert Mueller kuhusiana na uwezekano wa ushirika na pia kuzuwia sheria kuchukua mkondo wake, pamoja na juhudi kadhaa kama hizo pamoja na juhudi zinazoendelea katika bunge la Marekani.
Suala la Urusi limekuwa mwiba katika utawala wa Trump kwa muda wa miaka miwili iliyopita, na matamshi yake hayo yanaashiria kwamba bado haoni kosa kwa mgombea wa urais wa Marekani kukubaöli msaada kutoka taifa ya nje.