Wafanyabiashara Manyara washauriwa kusajili Majina BRELA



Na John Walter-Babati

Wafanyabiashara nchini wametakiwa kusajili majina ya biashara zao  kwa wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) ili kuepuka muingiliano wa Majina.

Akitoa semina kwa wafanyabiashara wa wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Suzana Senso  Kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa shirika la usajili wa Biashara na [BRELLA] ni fursa kwa mfanyabiashara kuweza kurasimisha biashara yake ili  waweze kupata fursa kutoka serikalini.

“Uzuri wa kujisajili kwenye Brela ni kwamba unaepuka muingiliano wa majina kwa kuwa tukishasajili jina moja hatwezi kulisajili kwa mara nyingine na pia unaepuka usumbufu unapotaka kupata kazi kutoka kwenye shirika au taasisi” alisema Senso.

Amesema BRELA imeanzisha Mfumo wa usajili wa biashara mtandaoni (OBRS) ili kuwawezesha watanzania popote wawapo kuweza kusajili majina ya biashara zao kwa kutumia mfumo wa computer, simu za mkononi, na tablet zilizounganishwa mtandaoni hivyo kuwaondolea usumbufu wa kutembelea ofisi za BRELA zilizopo Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya usajili wa majina ya biashara.

Ameongeza kuwa; Mfanyabiashara anapojisajili inamsaidia kutambulika kibiashara kwa kuwa atakuwa amerasimisha na kutambulika kisheria

Amesema madhara yanayoweza kumpata mtu ambaye hajasajili biashara yake ni pamoja na kutokutambulika hivyo kukosa oda kutoka sehemu mbalimbali.

Hata hivyo wajasiriamali na wafanyabiashara wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya mafunzo hayo kutoka Brela wamesema kuwa wapo tayari kusajili majina ya biashara zao baada ya kupata uelewa.

BRELA ilianzishwa na kuzinduliwa rasmi Desemba 9, 1999 chini ya wizara ya viwanda na biashara kwa sheria ya wakala za Serikali namba 30 ya mwaka 1997,ambapo majukumu yake makuu ni kusajili makampuni; kusajili majina ya biashara; alama za bisahra na huduma; kutoa hataza-Uvumbuzi kwa muda maalum (Patents of inventions) na kutoa leseni za viwanda na kusajili viwanda.
Mpya zaidi Nzee zaidi