Jeshi la Polisi lakanusha kuvunja Kongamano Zanzibar


Na. Thabit Hamidu, Zanzibar      

Muda Mchache mara baada ya kuvunjika kwa Kongamano liloandaliwa na Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja  limekanusha taarifa zinazozagaa kuwa wamehusika na kuvunja Kongamano hilo.

Akizungumza na kwa njia ya Simu na Muungwana Blog, Kamanda wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja, Thobias Gesauda Sedoyeka amesema kuwa Jeshi la Polisi hawakuuhusika kulivunja kongamano hilo ambalo limeratibiwa na kamati ya Maridhiano.

"Askari wa doria walikuwa katika majukumu yao ya kazi ya kila siku na kubaini kuwa kuna mikusanyiko mkubw wa watu ambapo wao walitaka kurudisha hali sawa,” alisema Kmanda huyo.

Alisema kuwa jeshi la Polisi halikumshikilia Maalim Seif na hayupo madem kama taarifa zinavyoelezwa kwa sasa Maalim Seif yupo nyumbani kwake.

“Ifahamike kuwa Jeshi la Polisi halikuhusika na kuzuia kongamano wala kumshikilia kiongozi huyo wa siasa,” alisisitiza Kamanda huyo.

Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuadhimisha miaka tisa ya kuasisisiwa kwa Serikali ya Maridhiano ambapo waratibu wa Kongamano hilo ni kamati ya maridhiano ikiongozwa na Hassani Nassoro Moyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi