Simba SC yapata kampuni ya kutengeneza jezi zake


Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya UHL Sport Dubai imeshinda tenda ya kutengeneza jezi za klabu ya Simba SC kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 ambapo klabu hiyo imeingia rasmi mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori, mkataba walioingia na UHL Sport kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo unafaida kuliko mikataba yote ya nyuma ambayo Simba imewahi kuingia.

"Thamani ya mkataba huu kwa miaka miwili ni Tsh. Milioni 600, hawa wanatupa vifaa vyenye thamani ya Tsh. Milioni 200 kwa msimu mzima," amesema Crescentius Magori.

Wakati huo huo Kikosi cha Simba SC kinaanza safari muda huu kurejea nchini kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kutoa burudani ya ukweli, burudani ya kibingwa katika Simba Day.
Mpya zaidi Nzee zaidi