ZFF yaongeza siku 5 za kufunga dirisha la Usajili



Na Thabit Hamidu,Zanzibar.     

Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar ZFF limesogeza mbele siku za kufunga Dirisha la Usajili Zanzibar kutokana na kile kinachodaiwa kuwa changamoto mbali mbali zilizojitokeza.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Afisa Hbari wa Shirikisho hilo Adam Natepe amesema kuwa ZFF imeongeza siku tano za ziada za usajili kutokana na Changamoto mbalimbali zilizojitokeza katik kipindi cha usajili.

“Dirisha la usajili Zanzibar litafungwa rasmi tarehe 06 mwezi wa 08 mwaka huu” alisema.
                                 
Natepe katika taarifa yake alifafanua kuwa ZFF imefanya maamuzi hayo kutokana kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika kipindi cha usajili jambo ambalo limeathiri utaratibu mzima uliowekwa.

“Mabadiliko hayo ZFF inavitaka vilabu kuitui fursA hiyo ipasavyo, kwani hakutakuwa na muda mwingine” alibainisha Afisa habari huyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi