Wahitihimu wa Elimu ya Juu watakiwa kuwaelimisha wenzao nchini



Na Thabit Hamidu,Zanzibar.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma amefanya mazungumzo na baadhi ya Wanafunzi wanaosoma na waliomaliza Vyuo Vikuu nchini China kwa lengo la kuleta maendeleo katika Elimu nchini.

Katika Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Mazizini Mjini Unguja, Waziri Pembe ameagiza kuitumia fursa walioipata kuwaelimisha vijana wengine ili nao waweze kuomba nafasi za masomo nje ya nchi kwa lengo la kuleta maendeleo nchini.

Amesema baadhi ya vijana wengi wanashindwa kuomba nafasi hizo kwa kuhofia kutojua lugha ya kiengereza.

Amesema katika nafasi hizo kumekuwepo mchanganyiko wa nchi mbalimbali na makabila tofauti ambapo baadhi yao hawajui kiengereza na kwa kiasi kikubwa wanazichangamkia fursa hizo.

Adha amesema pia kuna tabia  baadhi ya watu kuitumia mitandao ya kijamii kuzituma nafasi hizo za masomo za nje ya nchi ambazo wakati mwengine zimeshapita muda au kutokuwepo kabisa nchi husika, na hivyo kusababisha kuwapotezea muda na muelekeo kwa wanaoomba nafasi hizo.

Hata hivyo Mhe Riziki amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekuwa ikiziweka wazi nafasi mbalimbali za masomo za nje ya nchi kupitia  ndani ya tovuti yake pakufanya  mtandao wake wa kijamii (Facebook) ili kuwasaidia wale wote wanaohitaji kuomba nafasi hizo.

Aidha amewataka kuwa wazalendo na nchi yao kwa kurejea nchini wayakapomaliza masomo yao ili kulitumiki Taifa lao, kwani bado Zanzibar inahitaji wasomi  katika kuleta maendeleo katika kila fani.

Akizungumza kwa niaba ya wenziwe Mwenyekiti wa Tawi la CCM China ndugu Salum Mohammed Ramia amemuomba Mhe Riziki kuandaa siku Maalum ya Utamaduni kwa Vyuo vya Zanzibar kwani kutasaidia kuvitangaza vyuo hivyo nje ya Nchi pamoja na kukuza kiswahili ambao ndio miongoni mwa utamaduni wao.

Pia ameshauri kufanya kongamano la vijana litajalowashrikisha wanavyuo wote wa ndani na nje ya nchi kujadili masuala ya Elimu kwa ujumla ili kuleta ufanisi wa Elimu nchini.




Mpya zaidi Nzee zaidi