Askofu Pengo ang’atuka, mrithi wake ateuliwa


leo Agosti 15 Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis amekubali ombi la Mwadhama Polycarp Karnidali Pengo la kustaafu katika majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam na nafasi yake inachukuliwa na Askofu Mkuu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi.