Vifo vyafikia 89 ajali ya Lori la mafuta


Majeruhi saba wa ajali ya lori la mafuta ya petroli iliyoanguka na kulipuka mkoani Morogoro waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam nchini Tanzania wamefariki dunia kati 32 waliokuwepo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitalini hapo, Aminiel Aligaesha amesema kwasasa wamebaki majeruhi 25 kati ya 46 waliopokelewa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Hii ina maana kuwa waliofariki kutokana na ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita ya Agosti 10, 2019 mkoani Morogoro hadi leo ni 89.

Amesema kati ya majeruhi hao 16 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine tisa wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi maalum iliyotengwa kwa ajili ya majeruhi hao.

Aligaesha amesema madaktari wanaendelea kufanya jitihada kubwa kuokoa maisha ya majeruhi waliobaki.


Mpya zaidi Nzee zaidi