Kampuni ya China inayosimamia mradi wa SGR kuajiri Wakenya zaidi


Kampuni ya China inayosimamia reli ya SGR ya Kenya inapanga kuajiri Wakenya zaidi wakati inaongeza idadi ya wafanyakazi wake wenyeji.

Kampuni ya Afrika Star inayosimamia uendeshaji wa reli hiyo, imesema inaajiri wahudumu wa treni, makondakta, na wakaguzi wa mizigo, na wakarabati wa njia za reli na madaraja.

Baadhi ya nafasi za ajira zipo kando kando ya njia ya Nairobi Mombasa, ambayo inawavutia zaidi watalii, na nyingine zipo kwenye sehemu inayoendelea kujengwa kutoka Nairobi hadi Naivasha, hasa kwenye eneo la Suswa, Ngong na Mai Mahiu. Kampuni hiyo imesema waombaji wanaoishi katika maeneo hayo watapewa kipaumbele.

Mpya zaidi Nzee zaidi