Serikali yaunda Tume kuchunguza ajali ya moto Morogoro


Waziri Mkuu Kassi Majaliwa amesema ameunda tume kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo la ajali ya lori iliyosababisha vifo vya watu 69, na kusema watu ambao hawakuwajibika kwenye ajali hiyo watachukuliwa hatua.

Ametoa kauli hiyo Mjini Morogoro katika shughuli ya kutambua miili ya watu waliofariki kwenye ajali iliyotokea aubuhi ya jana.

"Hapa Manispaa kulikuwa na kitendo cha Fire, japo najua walikuja kwa kuzima, lakini je walikuja baada ya muda gani. kwa hiyo lazima tujiridhishe. Tumesisitiza umakini na uwajibikaji, nasikia tumeokoa mafuta sasa tumeokoa yakiwa yameisha, nitaunda tume ya wataalamu ili waniambie haya maswali madogo, majibu yake ni yapi", amesema Majaliwa.

Amendelea kwa kusema, "Je huu muda ambao walikutana hawa ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kwa ajili kutoa mafuta, ni nani aliwazuia, mimi ninajua trafiki huwa wanakuwa na haraka sana, ajali inapotokea, nani alihusika kuwazuia".