Loading...

8/16/2019

Kikosi cha Taifa Stars kujiandaa na Kombe la Dunia 2022 mbioni kutangazwa


Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndayiragije huenda akatangaza kikosi wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Burundi kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2022.

Mechi ya kwanza itachezwa Sept 4, 2019 Bunjumbura, Burundi na mchezo wa marudiano utachezwa Sept 8, 2019 Dar es Salaam.

"Mwalimu ameshaleta program yake kwa ajili ya mechi hiyo na anatarajia kutangaza kikosi wakati wowote kuanzia sasa kwa sababu tutatakiwa kuviandikia barua vilabu kwa ajili ya kuwaomba wachezaji angalau wiki mbili kabla ya wachezaji kuingia kambini" amesema Wilfred Kidao, Katibu Mkuu wa TFF.

Ameendelea kwa kusema "Wachezaji wanatarajiwa kuingia kambini tar 29 baada ya mechi za tar 28 na 28 lakini kuna changamoto ya wachezaji wanaotoka nje nje ambao mwalimu atawaita kwa sababu mfano Nahodha Mbwana Samatta atakuwa na mechi Sept 1 kwa hiyo anaweza akaunganisha moja kwa moja hadi Burundi na kuungana na wenzake."


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger