Shirikisho la soka nchini Morocco limefikia makubaliano na Vahid Halilhodžić aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Algeria hii ni baada ya kuachana na Harve Renard.
Morocco si kwamba walipenda kuachana na Renard bali yeye mwenyewe aliona kwamba ni wakati sahihi kwake kuondoka baada ya kupata dli nzuri zaidi ya kufundisha timu ya taifa ya Saudi Arabia.
Inasemekana kocha mpya wa Morocco atakuwa akilipwa €112,000 (zaidi ya Tsh. 280m) mshahara ambao utamfanya kuwa kocha ambaye analipwa fedha nyingi kuliko wote barani Africa.
