Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera leo amezindua tawi jipya na la kwanza katika mkoa wa Kilimanjaro la Viva Yanga-Kilimanjaro.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga,Saad Khimji pamoja na Mjumbe wa kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Kawina Konde pamoja na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.
Ikumbukwe Yanga SCwako mjini Moshi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakaochezwa kesho (Ijumaa) katika uwanja was Chuo kikuu Cha Ushirika mjini Moshi dhidi ya Polisi Tanzania.

