Mahujaji wahitimisha ibada ya Hijja katika mlima wa Arafa

Zaidi ya waumini milioni mbili wa dini ya Kiislamu kutoka pande tofauti za ulimwengu wamekusanyika leo kupanda mlima wa Arafa, karibu na mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Hatua hiyo ndio inaashiria kilele cha ibada ya Hijja. Serikali ya Saudi Arabia imewapeleka maelfu ya wana usalama katika njia zote za maeneo matakatifu ambazo zina umbali wa kilometa 20, mashariki mwa Makka.

Mahujaji wa kiume wamejitanda mavazi meupe, wakati wanawake wamevaa mavazi huru ambayo hayana mapambo wala vito.

Mlima huo wa Arafa ndio eneo mtume Muhammad alipotoa risala zake za mwisho takribani karne 14 zilizopita.
Mpya zaidi Nzee zaidi