Paul Pogba awatoa hofu Manchester United


Mchezaji wa Manchester United, Paul Pogba amewatoa hofu viongozi wa timu hiyo kutokana na baadhi yao kuamini kuwa anaweza asiwe na mchango chanya msimu 2019/20 kwa kudhani akili yake imehama.

Pogba alikuwa anahusishwa kwa karibu kuwa katika mipango ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na mwenyewe alishawahi kuripotiwa kuomba kuondoka ndani ya Man United lakini dili hilo lilishindwa kutimia.

Paul Pogba amewatoa hofu viongozi wake kuwa hawezi kuwa mfano mbaya katika timu na kushawishi vitu hasi kwa sababu tu jambo lake halijatimia na akili yake na fikra vitaendelea kuwaza kuitumikia Man United.