Waandishi wa habari wa Somali siku ya jana waliomboleza kifo cha mwenzao ambaye aliuawa wakati wa mapigano makali kati ya Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA) na wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabab katika mkoa wa kusini.
Shirikisho la Wanahabari wa Somali (FESOJ), umoja wa waandishi wa habari, lilisema Gacal Abdulle Gacal, ambaye alikuwa akifanya kazi na redio ya SNA alikuwa ni mmoja wa wale waliouawa wakati kundi la wanamgambo walivamia kituo cha jeshi katika mji wa Awdheegle.
"Tumesikitika sana kusikia kuwa mwenzetu Gacal alikuwa miongoni mwa waliofariki kutokana na mlipuko mkubwa katika kijiji cha Awdheegle," Mohamed Muse, mkurugenzi wa redio ya SNA alisema.
