Waziri aiomba Nethaland kushirikiana katika kukuza sekta ya Elimu nchini


Na Thabit Hamidu, Zanzibar

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma ameitaka Taasisi ya Kimaendeleo kutoka nchini Nadhalend NHHL, kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika miradi mbali Mbali yenye lengo la kuendeleza sekta ya Elimu nchini.

Akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo wakati alipofika ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga, Riziki Pembe  amesema mashirikiano hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa  katika kuimarisha udugu wa nchi mbili hizo.

Waziri Pembe amesema bado Zanzibar inakabiliwa na tatizo la upungufu wa madarasa ya kusomea hasa katika ngazi ya Maandalizi na msingi, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu  wapya wanoandikishwa Skuli kila mwaka.

Hivyo amesema bado Serikali pamoja na wafadhili mbalimbali wanaendeleza jitihada za kusaidia kujenga madarasa mapya ili kusaidia kupunguza tatizo hilo.

Aidha ameishukuru Taasisi hiyo kwa uamuzi waliochukua kuamua  kujenga Skuli ya Maandalizi na Msingi Zanzibar ambapo amemuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na mbalimbali wakiwemo wa Elimu ili kuleta maendeleo nchini.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimaendeleo kutoka Nchini Nadhalend NHHL,Ayhan Arslantas amesema amefarajika kufika Zanzibar kutokana na mashirikiano mazuri aliyoyapata ambapo ameahidi kuendelea kujenga Skuli katika sehemu nyengine ili kuendeleza Elimu Zanzibar.

Taasisi ya Kimaendeleo kutoka nchini Nadhalend NHHL tayari imeshajenga Skuli ya Maandalizi na Msingi inayojuilikana VIVID DREAMS na kufunguliwa na Waziri wa Elimu na na Mafuzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki  Pembe Juma huko Mbuzini Wilaya ya Magharibi A, Unguja.



Mpya zaidi Nzee zaidi