Fahamu kuhusu usimamizi wa fedha katika biashara

Moja kati ya elimu muhimu kwa kila mtu ambaye ameamua kufanya biashara ni elimu ya usimamizi wa fedha. Fedha inahitaji usimamizi wa hali ya juu ili iweze kuongezeka na kutimiza malengo uliyonayo katika biashara yako.

Unapokosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha inaweza kuzalisha matatizo kadha wa kadha katika biashara yako. Baadhi ya matatizo yanayoweza kutokea kwenye biashara yako kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri wa fedha.

Unaweza kupata hasara katika biashara yako.
Unaweza kupunguza kiasi cha mtaji wako.
Unaweza kuingia kwenye mgogoro wa madeni.
Unaweza kushindwa kununua mali ghafi kwaajili ya uzalishaji.
Unaweza kupoteza thamani ya jina la biashara yako.
Unaweza kupunguza thamani ya ubora wa bidhaa zako.

Kuna matatizo lukuki ambayo yanaweza kujitokeza kwasababu ya kukosa usimamizi mzuri kwenye masuala ya fedha hivyo elimu ya masuala ya usimamizi wa fedha ni muhimu sana katika biashara yako.

Usimamizi wa fedha ni nini ?
Usimamizi wa fedha ni namna ya kusimamia mapato na matumizi katika biashara ili kutimiza lengo fulani.

Mapato ni fedha inayoingia katika biashara yako kupitia mauzo.

Matumizi ni fedha inayotoka katika biashara yako kupitia malipo.

Biashara yoyote ni lazima iwe na lengo (objective) ili uweze kuwa na ufanisi katika hiyo biashara. Huwezi kuwa makini katika biashara kama hujui unahitaji kutimiza nini.

Mpango kazi wa biashara ( Business Plan) ni kitu cha muhimu sana kwa kila mfanya biashara ambaye anataka kuleta mageuzi makubwa katika uchumu wake binafsi na jamii inayomzunguka.

Unapoweka kwenya matendo elimu ya usimamizi wa fedha inatakusaidia kutimiza malengo ulinayo katika biashara yako.

Kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kutengeneza mfumo wa usimamizi wa fedha katika biashara yako.

 BAJETI ni mpango wa kifedha unaonyesha makisio ya mapato na matumizi katika biashara ndani ya kipindi fulani.

Katika bajeti kuna vipengele viwili vya muhimu ambavyo unapaswa kujua kwa kina ili uweze kutengeneza bajeti yenye kukidhi vigezo.

i/ Mapato
ii/ Matumizi
iii/ Muda maalum.

MAPATO;
Mapato katika baishara hutokana na mauzo ya bidhaa au huduma. Kama unaona mapato yako ni kidogo katika biashara yako fikiria ni bidhaa gani au huduma gani ambayo unaweza kuongeza ili kuongeza mauzo katika biashara yako, unapoongeza mauzo moja kwa moja utaongeza mapato na kiasi cha faida.

Kwa mfanyabiashara anayeanza biashara ni vema ukajua chanzo cha mtaji wako ni nini ili kukusaidia kufanya makadirio vizuri.

MATUMIZI;
Matumizi hutokana na malipo unayofanya katika biashara yako mfano kununua malighafi, kulipia pango kwaajili ya baishara, kuwalipa wafanyakazi, kulipia usafari kwaajili ya kusafirisha bidhaa nk.

Unatakiwa kuainisha matumizi ya baishara yako vizuri na ni vema ukatofautisha matumizi yako binafsi na matumizi ya biashara.

Changamoto kwa wafanyabaishara ni kuchanganya matumizi yao binafsi na matumizi ya biashara mfano unakuta mtu anatao fedha ya kununulia simu binafsi kutoka kenye baishara halafu baadae anajiuliza kwanini baishara yake haikui.

Unapotoa fedha kwenye biashara kwa matumizi binafsi bila kurudisha tarajia mambo haya kutokea kwenye biashara yako.
Faida kupungua.
Mtaji kupungua
Kupata hasara.

MUDA MAALUM;
Ni lazima bajeti iandaliwe ndani ya muda maalum au kipindi fulani. Bajeti inaweza kuandaliwa kwa juma, mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na hata mwaka mzima.

Bajeti inaonyesha makadiro ya mapato ndani ya kipindi fulani hivyo unakuwa na taswira ya mapato ya baishara ndani ya huo muda maalum.