Na Timothy Itembe, Mara
Mkuu wa Wilaya Tarime Mkoani Mara,Charles Kabeho ameikuimbusha Halmashauri ya Wilaya Tariome kujenga miundombinu ya Gereza la Tarime ili wafungwa na mahabusu wapate mahali pazuri pa kujisitiri.
Kabeho alisema jana katika kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi katika ukumbi wa halmashauri hiyo kuwa kuna haja halmashauri kuunga juhudi za Raisi awamu ya Tano John Pombe Magufuli katika kuboresha miundombinu ya Gereza ili wafungwa pamoja na mahabusu wakapate mahali pazuri pa kujisitili.
Kwa upande wake Diwani kata ya Bumera,Deougatius Ndege CCM alisema kuwa halmashauri ya Tarime Vijijini ilishatenga bajeti kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ya Gerza hilo.
“Kabla mkuu wa wilaya hajaliona hili halmashauri yangu pamoja na madiwani tulikuwa tumekwisha liona ndio sababu baraza liliazimia kutenga bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya Gerza la Tarime ambalo kwa ujumla likahudumia halmashauri tatu kwaana ya Tarime vijijini,Tarime mjini pamoja na halmashauri ya Rorya”alisema Ndege.
Naye Diwani kata ya Kemabmo kupitia chama cha mapinduzi CCM,Rashid Bogomba alisema kuwa yeye binafsi akiwa amekamata na kupelekwa Gerezani hapo alichangia vigae pamoja na mifuko ya Simenti kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Choo kilichoharibika ndani ya gereza pamoja na minundombinu mingine lakini hadi sasa hakuna kilichoendelea.
Bogomba alitumia nafasi hiyo kumuomba mkuu wa wilaya Tarime Charles Kabeho pindi fedha hizo zitakapotolewa na kwenda Gerezani afuatilia kwa ajili ya utekelezaji ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
Apoll Tindwa ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijini alikiri halmashauri yake kutenga bajeti kwa ajili ya kurekebisha na kuboresha miundombinu ya Gereza hilo ambao amesema kuwa kinachosubiriwa ni upatikanaji wa fedha ili kupelekwa kwaajili ya utekelezaji.
