Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema nchi yake kesho itatangaza hatua mpya za kupunguza ahadi zake kwenye makubaliano ya nyuklia, licha ya juhudi za kidiplomasia kutaka vikwazo vya Marekani Kulegezwa.
Iran pamoja na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinafanya mashauriano kuunusuru mkataba huo uliofikiwa mwaka 2015 lakini ambao umekumbwa na mtikisiko tangu Marekani ilipojitoa mwezi Mei mwaka uliopita.
Juhudi hizo zimekuwa zikiongozwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye amekuwa akijaribu Kuishawishi Marekani kulegeza baadhi ya vikwazo vyake vinavyoidhofisha Iran.
Rais Rouhani amenukuliwa na tovuti ya ikulu akisema hafikirii kuwa watapata makubaliano, kwa hivyo watachukua hatua ya tatu na wataitangaza maelezo kesho.