Johnson ameliambia bunge kuwa muswada huo wa upinzani utakaowasilishwa bungeni leo, utahujumu uwezo wa nchi hiyo kufanya mashauriano mapya na Umoja wa Ulaya.
Johnson amesema angali ana imani kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya watakubaliana kuondoa kipengee chenye utata kuhusu mpaka wa Ireland maarufu kama “backstop” kwenye makubaliano yao.
Kipengee hicho kinalenga kuweka wazi mpaka kati ya Ireland kaskazini na jamhuri ya Ireland baada ya Brexit.
