https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kituo cha msaada wa kisheria chalia na fumo dume Mbinga | Muungwana BLOG

Kituo cha msaada wa kisheria chalia na fumo dume Mbinga



Na Ahmad Mmow, Mbinga.

Kutokana na fikra za mfumo dume walizonazo wanaume wengi wilayani Mbinga, jitihada zaidi za kutoa elimu ya sheria kwa jamii inahitajika wilayani humo.

Hayo yameelezwa na mratibu wa kituo cha msaada wa kisheria cha wilaya ya Mbinga( NAJATA), Daniel Chindengwike alipozungumza na Muungwana Blog, leo mjini Mbinga.

Alisema kituo hicho kinapokea mashauri mengi yanayohusu mirathi na ndoa,idadi kubwa ya wanaolalamika ni wanawake kutokana na kudhulumiwa mali baada ya kufariki waume zao au ndoa kuvunjika.

Alisema kutokana na hali hiyo kituo hicho kimebaini kwamba sababu kubwa ya wanawake kudhulumiwa ni wanaume kujiona wanahaki zaidi kuliko wanawake. '' Mfumo dume katika wilaya hii bado upo, wanaume wengi wanaamini kwamba mwenye mali ni mwanaume. Mwanamke hana haki kabisa. Wanaume wengi hawawashirikishi wakezao kupanga matumizi ya fedha na mali za pamoja. Hata wakiuza kahawa na mazao mengine hawawashirikishi, ndipo kunahaja kufanyika jitihada kubwa ya kutoa elimu,'' alisema Chindengwike.

Mratibu huyo alisema fikra za kuona wanaume wanahaki kuliko  wanawake inasababisha hata wajane kunyang'anywa mali na ndugu za marehemu. Huku wajane hao wakiachiwa kulea watoto wa marehemu ndugu yao.

Chindengwike alitoa mfano wa wanawake wawili kati ya wengi ambao kituo hicho kimewasaidia kupata haki zao ambazo walidhulumiwa kutokana na mfumo dume kuwa ni  Osana Nchimbi wa kijiji cha Sepukila na Orester Komba wa mtaa wa Mjimwema katika mamlaka ya mji wa Mbinga. '' Osana baada ya kufariki mume wake alifukuzwa na kunyang'anywa nyumba mbili zote ambazo alijenga na marehemu muwe wake, pamoja na mashamba yote.

Nae mume wa Orester aliuza nyumba na vyombo bila kumshirikisha Orester kwamadai mali hizo za pamoja zilikuwa zake yeye peke yake na hakumgawia hata shilingi moja kabla ya mahakama kumuamrisha amgawie Orester nusu ya fedha za mauzo ya gari na vyombo navyo wakagawane. Kumbe mahakama wakati inatoau uamuzi huo hata hivyo vya  ndani alikuwa ameuza,''alisema Chindengwike.

Kwaupande wake mwanasheria wa shirika la msaada wa kisheria la AICIL ambalo linaratibu na kusimamia kazi za vituo vya kisheria vilivyopo mkoani Ruvuma, Thomas Thomas alikiri kwamba tatizo la mfumo dume nikubwa mkoani humo.

Kwani migogoro ya mirathi, ndoa na ardhi inaongoza. Migogoro ambayo chanzo chake ni mgao wa mali.