Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuachana na mpango wake wa kufanya kilele cha mkutano wa mataifa ya G7 wa mwaka 2020 katika hoteli yake ya Miami.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Trump alisema kutokana na vyombo vya habari na wanachama wa Demokrat kulichukulia tofauti sana suala hilo ameamua kuachana na mpango wake wa kufanya mkutano huo katika hoteli yake ya Miami.
Trump aliandika "Hatuzifikirii tena Trump National Doral wala Camp David kwa ajili ya G7, 2020. Tumeshaanza kutafuta sehemu nyingine."
Ijumaa iliyopita katibu wa ikulu ya Marekani, Mick Mulvaney alitangaza katika kikao cha wanahabari kwamba mkutano wa G7, 2020 utafanyika katika hoteli ya Trump iliyopo Miami.
Uamuzi huo ulipingwa vikali na wakosoaji wengi ukisemwa kwamba ni kinyume cha maadili.