Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limewataka wateja wake kuwa wazo kwa hisia zao, ili maswali, maoni na hoja zao mbalimbali zijibiwe na Shirika kwa lengo la kuimarisha huduma zitolewazo na Shirika hilo, ambapo ‘Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani’ imekuja na Kauli Mbiu “ Sema na NSSF”, inayowapa nafasi wateja kusema kero zao
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, wiki hii Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio alisema kuwa wanatumia kauli mbiu hiyo ikilenga kuwasikiliza wanachama na wateja wao kubaini hisia na changamoto zao juu ya mafao pamoja na huduma zingine zinazotolewa na NSSF ili kuimarisha huduma zao.
“NSSF tunatoa huduma kwa wateja ndani ya wiki hii ya huduma kwa wateja ulimwenguni kwa hiyo tuko hapa leo kuhakikisha tunatoa huduma iliyobora kwenye siku hii; na siku zijazo kama kawaida yetu, tayari tunamkataba wa huduma kwa wateja ambao tunatakiwa kufuata ili kuendeleza huduma bora kwa watu waweze kufurahia huduma zetu”, Bw.Erio
