EWURA yafanikiwa kudhibiti uchakachuaji Mafuta

Mamlaka ya Udhibiti ya Nishati na Maji,Energy and Water Utilities Regulatory Authority[EWURA] imefanikiwa kudhibiti Uchakachuaji wa Mafuta kutoka asilimia 74% kwa mwaka 2007 na hadi kufikia asilima 4% pekee kwa mwaka huu 2019.

Hayo yalisemwa  Novemba 1,2019 na Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo,Bw.Zinyangwa Mchani wakati akitoa wasilisho la Mamlaka hiyo kwenye semina na waandishi wa Habari jijini Dodoma.


Bw.Mchani ambaye pia ni mkurugenzi wa Uchumi EWURA amesema hiyo ni kutokana na sera nzuri ya Mamlaka hiyo ilivyojipanga kwa sasa pamoja na utendaji maridadi wa wafanyakazi wake na kuongeza kuwa uchakachuaji wa Mafuta ilikuwa changamoto kubwa hapa nchini.

Aidha,Bw.Mchani amesema EWURA imeokoa jumla ya Tsh.Bilioni 121.6 kwa mwaka 2012 na 2013 hali imetokana na kuandaa na mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja.

Katika hatua nyingine Bw.Mchani amesema ,ili kukabiliana na Upungufu wa Mafuta hususan maeneo ya Vijijini EWURA imeanzisha kuruhusu mfumo wa Vituo vya mafuta vinavyo vinavyotembea .

Ameendelea kufafanua kuwa,EWURA imefanikiwa kutoa Leseni 1561 za biashara ya Mafuta ,ambapo leseni za biashara za jumla ni 66 na rejareja ni 1397.

Kuhusu suala la Maji ,Kaimu Mkurugenzi huyo wa EWURA amesema mamlaka hiyo imekuwa na changamoto ya kudhibiti mamlaka za maji 130 kati ya hizo 95 ni za Wilaya hivyo inakuwa changamoto kubwa katika uendeshaji
wake.

Hata hivyo,EWURA Mnamo Tarehe 8,Juni,2015 ilishinda tuzo ya ya Energy ya Regulator of the Year Award.

Ikumbukwe kuwa EWURA ilianzishwa kwa Mujibu wa Ibara ya 4 ya Sura ya 414 ya sheria ya Tanzania na ilianza kufanya kazi Septemba ,2006 kwa dhumuni la kudhibiti huduma za nishati,[Umeme,Petrol, na Gesi asilia]na Maji na Usafiri huku ikiwa na Majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia masuala ya leseni