Loading...

11/03/2019

Chelsea ya Lampard yazidi kutakata

Mshambuliaji Tammy Abraham akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la pili dakika ya tano katika ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya Watford kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Vicarage Road.

Bao la pili la Chelsea lilifungwa na Christian Pulisic dakika ya 55, kabla ya Gerard Deulofeu kuwafungia wenyeji kwa penalti ya msaada wa Marudio ya Picha za Video (VAR) dakika ya 80.
Loading...