Loading...

1/16/2020

Dart yatoa taarifa kuhusu huduma ya mabasi ya mwendokasi


Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka, maarufu kama Mwendokasi (DART), wamewataka abiria wote wanaotumia mabasi hayo, kutoka maeneo ya Kimara kuelekea mjini kuwa watumie mabasi hayo hadi Morocco na wakishafika hapo, wachukue usafiri mwingine utakaowafikisha mjini.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 16, 2020, hii ni kufuatia uwepo wa mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, iliyopelekea eneo la Jangwani kujaa maji na hivyo barabara hiyo kutopitika.

"Tunawashauri wasafiri wa mabasi ya Mwendokasi wanaotokea Kimara kuelekea mjini-kati kuwa watumie mabasi hayo mpaka Morocco, halafu wachukue usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka mjini-kati, Kariakoo na sehemu nyingine za jiji. Hivyo hivyo, wale wanaotokea mjini-kati kwenda Kimara, wachukue usafiri mbadala mpaka Morocco ambapo wanaweza kuendelea na usafiri wa mabasi ya Mwendokasi kuelekea Kimara" imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imeeleza kuwa mvua iliyonyesha leo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, itaendelea kunyesha hadi kesho Januari 17, 2020.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger