Ifahamu historia ya rapa Eminem

Oktoba 17, 1972 alizaliwa rapa maarufu wa Marekani ambaye amekuwa akifahamika kwa jina la Eminem.

Huyu ni mtunzi wa nyimbo, mwimbaji, prodyuza, muongozaji wa filamu na mwigizaji. Amekuwa akichukuliwa kuwa rapa ambaye ametulia katika kadhia hiyo kwa muda mrefu bila kuyumba. Jarida la Rolling Stone liliwahi kumuita King of Hip Hop. Jina lake halisi ni Marshal Bruce Mathers III alizaliwa huko St. Joseph, Missouri nchini Marekani. Ni mtoto pekee wa Marshall Bruce Mathers Jr. na Deborah Rae au Debbie. Ana asili kutoka Uingereza, Uskochi, Ujerumani, Uswisi, Poland na Luxembourg.

Mama yake alitaka kupoteza maisha saa 73 kabla ya kujifungua kwa Eminem. Wazazi wake walikuwa waimbaji kati bendi ya muziki ya Daddy Warbucks ambayo ilikuwa ikifanya kazi zake katika ukumbi wa Ramada Inns karibu na mpaka wa Dakotas-Montana kabla ya maeneo hayo kutenganishwa. Makuzi ya Eminem yamekuwa ya taabu kwani wazazi wake walitengana, ikambidi Eminem amfuate mama yake ambapo walienda kuishi Michigan na Missouri walikokuwa wakikaa katika nyumba moja kwa miaka miwili. Wakiwa Missouri waliishi maeneo mengine kama St. Joseph, Savannah na Kansas City.

Baba yake alipata mwanamke mwingine huko California na kumzalia watoto. Akiwa kijana Eminem alimwandikia barua baba yake, katika barua hiyo Debbie alimwambia yote kuhusu maisha yao. Katika ujana wake Eminem aliishi katika jamii ya watu weusi, wafanyakazi katika maeneo mbalimbali kama vibarua kwa ajili ya kujipatia riziki hususani maeneo ya jirani na Detroit.

Katika maisha hayo Eminem alikuwa akipigwa na vijana wenzake wenye asili ya Afrika (Black Americans) kutokana na hali iliyokuwepo wakati huo ya wazungu kuwabagua Wamarekani Weusi hivyo kumuona Eminem katika mitaa yao ilikuwa kama kejeli fulani.

Akiwa mtoto Eminem alikuwa akipenda kusoma vitabu vya hadithi akitamani kuwa msanii wa vichekesho kabla ya kupenda zaidi Hip Hop. Alianza kupata ushawishi wa Hip Hop kutoka kwa Tracy Lauren Marrow maarufu Ice-T kibao cha Reckless ambao alipewa na kaka yake Ronnie Polkingharn licha ya kutozaliwa kwa baba mmoja lakini kwa kiasi kikubwa baadaye alikuwa mwalimu wake aliyemtia moyo katika muziki huo Hi Hop.

Kaka yake huyo alijiua mwaka 1991. Akiwa na miaka 14 Eminem alianza kurap akiwa na rafiki yake waliyekuwa wakisoma shule wote Mike Ruby ambaye ni maarufu sana kama Manix na baadaye M&M alipomwingiza na Eminem. Akiwa huko alikuwa akipambana na kundi jingine la wanafunzi marapa kila jumamosi ilikuwa ni freestyle na kuandika. Albamu yake ya kwanza ilikuwa ni Infinite ya mwaka 1996. Mpaka sasa ametoa albamu 10 mwaka 2018 alitoa albamu aliyooiita ‘Kamikaze’. Hadi sasa ameuza nakala milioni 230 duniani kote ya album zake na kuweka rekodi ya kuwa Msanii wa zama zote aliyeuza zaidi. Mwaka 2000 aliweka rekodi ya kuwa msanii bora katika mauzo ya kazi zake nchini Marekani. Ameshinda tuzo 15 za Grammy, tuzo 8 za American Music, tuzo 17 za Billboard, MTV Europe pia tuzo moja ya Academy.