Na John Walter
Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, akihitimisha safari ya miaka 23 iliyomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la kimataifa.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 41, ametangaza uamuzi huo kupitia ujumbe wa video aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi, akisema amefikia wakati wa kukabidhi jezi namba saba aliyokuwa akiitumia akiwa na timu ya taifa.
Katika kipindi chake, ameiwakilisha Ureno katika mashindano sita ya Kombe la Dunia, akishinda pia taji la Ubingwa wa Ulaya (EURO) na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika soka la kimataifa kwa upande wa wanaume.
Kwa upande wake, Shirikisho la Soka la Ureno limetoa pongezi na shukrani za dhati kwa Ronaldo kutokana na mchango wake kwa taifa hilo, likisema linapanga kuandaa hafla maalumu ya kumuenzi ili mashabiki na wananchi wapate fursa nyingine ya kumshangilia na kusherehekea mafanikio yake.
