Watakiwa kupima homa ya ini pamoja na virusi vya ukimwi



Na Hamisi Abdulrahmani,Masasi

Watumishi wa Serikali na taasisi binafsi Mkoani Mtwara wamehimizwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ikiwemo ugonjwa wa homa ya ini( Hepatitis-B) pamoja na virusi vya Ukwimwi ili kujua hali halisi ya afya kisha kuchukua hatua za matibabu zaidi.

Wito huo ulitolewa jana wilayani Masasi Mkoani hapa na mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Gelasius Byakanwa alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Sekretarieti Mkoa wa Mtwara katika mkutano wao mwaka uliofanyika kwenye katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Masasi.

Alisema suala la upimaji wa afya kwa kila mmoja lazima liwe ni utamaduni kwa watumishi wa serikali, taasisi binafsi na jamii kwa ujumla.

Alisema kwa sasa kumekuwa na tatizo la ugonjwa wa ini ambao umeshika kasi kubwa kwa jamii hasa ndani ya mkoa wa Mtwara.

Alisema Baraza la wafanyakazi la Sekretarieti Mkoa wa Mtwara pia wanaowajibu wa kuhamasisha wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kupima afya hasa homa ya ugonjwa ini na virusi vya ukimwi.

Byakanwa alisema kila mmoja akiwa na tabia ya utamaduni wa kupima afya kutakuwa na faida nyingi za kiafya ikiwemo kujua hali halisi ya afya na kuweza kuchukua hatua za nini cha kuchafanya.

Alisema ugonjwa wa homa ya ini umekuws tishio kwa jamii na umekuwa ukiwakumba watu wengi kwa sasa hivyo watu wakiwa mwamko wa kupima ugonjwa itakuwa bora kws afya zao.

Byakanwa alisema moja ya faida moja wapo ya kupima homa ya ini( Hepatitis-B) kwanza kufahamu kama mtu ameambukizwa au hana ugonjwa huo.

Alisema iwapo mtu atakuwa ameambukizwa ni pamoja na kuanza matibabu lakini kama mtu atakuwa hajaambukizwa basi anatakiwa kufanya njacho ya kudhibiti ugonjwa huo.

"Tukapime afya zetu lakini pia tupime homa ugonjwa wa ini( Hepatitis-B) lakini ugonjwa wa ukimwi ili tujuwe hali halisi ya afya zetu,"alisema Byakanwa

Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa serikali mkoani Mtwara haitofurahishwa kuona watu wake wakiathiliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo homa ya ini pamoja na virusi vya ukimwi.

Alisema nguvu kazi ya wananchi wa Mtwara bado inahitajika kwa ajili ya kuijenga Mtwara na kuweza kupiga hatua ya kimaendeleo.