Baadhi ya Raia wa Misri wamelaani kitendo cha Rais wa zamani wa Nchi hiyo Hosni Mubarak kuzikwa kwa heshima ya kijeshi hapo jana huku wakisema hakustahili heshima hiyo kutokana na kuitawala Misri kidikteta.
Mubarak aliitawala Misri kwa miaka 30 hadi pale alipoondolewa kwa maandamano ya Wanachi mwaka 2011.
Mizinga imepigwa na jeneza lake limebebwa kwenye msafara wa farasi kuashiria mafanikio ya Mubarak enzi za vita, Rais wa sasa wa Misri Abdel Fatah al-Sissi, alihudhuria pia mazishi.
Mubarak amezikwa kwenye eneo la makaburi ya familia yake la Heliopolis, Cairo.
