Loading...

3/23/2020

China yatoa tangazo kuhusu ndege zote za abiria zinazokwenda nchini humo

Serikali ya China imetangaza kuanzia leo ndege zote za abiria zinazokwenda nchini humo katika mji mkuu wa Beijing, zitalazimika kushukia katika viwanja vya ndege vya miji na majimbo ya jirani ili abiria wafanyiwe uchunguzi wa afya kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Beijing.

Abiria watakaosafiri na Shirika la Ndege la Ethiopia watashukia katika Uwanja wa Ndege wa Taiyuan (TYN) na abiria watakaosafiri na Shirika la Ndege la Emirates watashukia Shanghai kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger