https://monetag.com/?ref_id=TTIb Dkt. Kawambwa akabidhi viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu | Muungwana BLOG

Dkt. Kawambwa akabidhi viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa amekabidhi viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu wa miguu katika jimbo lake.

Akizungumza wakati wa kukabidhi viti mwendo hivyo, Dkt. Kawambwa alisema kuwa, viti mwendo hivyo ni msaada kutoka kwa mama Janeth Magufuli hivyo anakabidhi kwa walengwa ili kutimiza wajibu wake kama alivyooagizwa na mama Janeth Magufuli.


Alisema Viti mwendo hivyo vitawasaidia watoto hao kutembea sehemu mbali mbali kwa kuendesha wenyewe au kuendeshwa na kuondoa usumbufu wa kuwabeba hata pale wanapokuwa na safari za lazima kama vile Hospitali Nk.

Aidha, aliwataka wazazi na walezi kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kuwahudumia watoto hao kwa muda mrefu zaidi jambo ambalo litampa moyo yule aliyetoa na kufikiria kutoa msaada mwingine.


Katika hatua nyingine Mbunge huyo wa Jimbo la Bagamoyo aliwashauri kina mama wenye watoto walemavu kuunda kikundi na kukisajili ili waweze kupatiwa mikopo ya serikali inayotolewa kwa vikundi.

Alisema serikali haiwezi kusaidia wananchi mmoja mmoja hivyo ni vyema wakiwa kwenye kikundi ili waweze kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ambayo haina riba na kwamba itawasaidia kujiendeleza kulingana malengo watakayojiwekea.

Dkt. Kawambwa alitoa rai hiyo baada ya kina mama wenye watoto walemavu kumuomba awasaidie wapate mitaji kwa ajili ya biashara ili kukabiliana na malezi ya watoto hapo.

Kwa upande wao wazazi na walezi wa watoto hao walimshukuru Mbunge huyo kwa kufikisha viti hivyo kama alivyokabidhiwa na mama Janeth Magufuli.