Loading...

3/21/2020

TFF kuwasimamisha wachezaji watakao vuka mipaka ya Tanzania

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia,  amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni wanaotumika ndani ya Tanzania iwapo wataondoka nchini hawataruhusiwa kurudi tena nchini kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona.

Karia amesema kuwa, Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari kwa ajili ya Virusi vya Corona hivyo wanaondoka na kwenda nje ya nchi huko hawatambui aina ya maambukiza yapo kwa kiasi gani.

"Hawajapewa likizo wachezaji bali ligi imesimama kwa ajili ya tahadhari ambayo inachukuliwa kwa sasa, kwa wachezaji wa kigeni watakaokwenda kwenye nchi zao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

"Tutawasiliana na mamlaka husika ili kuona namna gani tutawazuia na hawataweza kushiriki kwenye ligi iwapo hali itatulia kwani tahadhari kuchukuliwa ni muda wote na sio muda mfupi," amesema.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger