Kuondolewa kwa majeshi ya Marekani kutoka Afghanistan kunaendelea kabla ya muda uliopangwa, afisa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP, wakati rais Donald Trump akirudia miito kwa wizara ya ulinzi kuwarejesha wanajeshi nyumbani.
Hatua hizo zinakuja wakati maswali kadha yanajitokeza kuhusiana na awamu ijayo ya vita vya muda mrefu vya Afghanistan, baada ya kumalizika kwa siku tatu za kusitisha mapigano na wakati wenye shauku wa kusubiri kuona iwapo ghasia zinaweza kurejea.
Chini ya makubaliano yaliyotiwa saini na Marekani na kundi la Taliban mwezi Februari, wizara ya ulinzi ilitakiwa kupunguza idadi ya wanajeshi kutoka 12,000 hadi 8,600 itakapofika katikati ya mwezi Julai, kabla ya kuwaondoa wanajeshi wote ifikapo Mei mwaka 2021.
Lakini afisa mwandamizi wa jeshi alisema idadi ya wanajeshi tayari ni kiasi ya 7,500, wakati makamanda wanaharakisha uondoaji wanajeshi kwasababu ya hofu ya janga la virusi vya corona.