Na Faruku Ngonyani , Mtwara.
Kuelekea uchaguzi Mkuu Tarehe 28 Oktoba 2020 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amewasihii wananchi wa Wilaya hiyo kuchagua viongozi wenye sifa na watakaleta maendeleo katika maeneo yao.
Ameyazungumza hayo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata za Nanguruwe , Moma , mbawala na kitere wakati wa kusikiliza na kutatua kero zao.
Adha amewasihii wananchi hao kuacha kuwachagua viongozi wanaotoa rushwa huku akisistiza kuwa kiongozi mwadilifu hatotokana na utoaji wa Rushwa.
Lakini pia Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa ili kupata maendeleo yenye tija katika maeneo yao na ni vyema wananchi wakamchagua kiongozi atakayeweza kusimamia na kuleta maendeleo ya kweli.
“Nawaomba wananchi msitumike vibaya utakuta mtu anakupa pesa shilingi elfu hamsini au anakupa dera kwahiyo wewe thaamani yako ni dera tu ?”
Kwa kuongeza Mkuu huyo wa Wilaya amewasihii wananchi wa kata hizo kuhakikisha wanadumisha amani na kuimarisha ulinzi na usalama kwa maeneo yao.
