Madiwani wapya 13 wachomoza Bagamoyo



Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

Madiwani wapya 13 wamechomoza Katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutoka kwenye Kata 13 kati ya 26 zilizopo ndani Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Madiwani hao wametoka kwenye Kata 26 zilizogawanyika katika Majimbo mawili ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo Chalinze lina Kata 15 wakati Bagamoyo kukiwa na Kata 11.

Zoezi hilo lililofanyika Julai 25, jimbo la Bagamoyo lenye Kata 11, nne zimepata sura mpya ambazo ni Makurunge, Kiromo, Dunda na Mapinga, huku Chalinze lenye Kata 15 Kimange, Mkange, Mandera, Mbwewe, Ubena, Bwilingu, Talawanda, Pera na Vigwaza zikipata sura mpya.

Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho, Katibu wa (CCM) Gertruda Sinyinza alisema kuwa zoezi hilo lililofanyika kwenye Kata, zimeratibiwa na Wenyeviti na Makatibu wa chama hicho, chini ya wasimamizi waliosimamia mchakato huo.

Akianzia na Kata ya Makurunge, Hamisi Seif kura 51, dhidi ya mtetezi Kabile Paul 25, Kata ya Kiromo Salumu Mikigo 58, Jitihada Mwinyimkuu 27 huku Hassan Wembe akishindwa kutetea nafasi hiyo, Kata ya Fukayosi Ally Ally amerejea kwa kura 96 mbele ya Msunye Manyakala 7.

Kata ya Yombo Mohamed Usinga 66 dhidi ya 6 za Abdallah Rashid, wakati Apsa Kilingo akitoka Viti Maalumu ameshinda Kata ya Dunda kwa kura 88 dhidi ya 69 za Dickson Makamba, huku
Said Ngatipula Kata ya Kerege ametetea kwa kura 57 dhidi ya Abasi Salehe 43.

Kata ya Mapinga Chandika Dismas 51, Shaaban Athumani 47 ambapo mtetezi Ibrahimu Mbonde hajagombea, Kata ya Zinga Mohamed Mwinyogogo amerudia tena kwa kura 33 dhidi ya Ally Sudi Ubaya na Hashimu Mwintanga.

Kata ya Nianjema Abdul Pyalla ametetea kwa kura 56 dhidi ya Rajabu Maliki 51,  Kata ya Magomeni Mwanaharusi Jarufu 90 dhidi ya 11 za Kisina Siajabu, Kisutu Aweso Mhidini amerudi kwa kura 57 dhidi ya 3 za Idrisa Salum.

Jimbo la Chalinze akianzia Kimange Ismail Msumi 50, Hussein Hemedi 29 huku mtetezi Hussein Hading'oka kura 21, Kata ya Mkange Mohamed Gelegeza 85, Abdallah Mwindad 67, Wema Mzenzi 57, Juma Mgweno aliyetetea 37 na Ally Majimengi 25.

Kata ya Mandera Madaraka Mbode ameshindwa kutetea kwa kupata kura 26, mbele ya Leon Mgweno 37 na Hashimu Salehe 28, Kata ya Msoga Hassani Mwinyikondo erejea kwa kura 68 wakati Mohamed Mzimba akikusanya 51.

Omary Habass ameng'ara Kata ya Mbwewe kwa kura 55, Omary Mhando 52 wakati Ramadhani Mahamba aliyetetea akipata 39, huku Kata ya Kibindu Ramadhani Mkufya amerejea kwa kura 87 dhidi ya Said Msami 54,

Kata ya Msata Selestine Semiono ameshinda tena kwa kura 154 akimwacha diwani wa zamani Shaaban Mtambo kura 48, wakati Kata ya Ubena Grofrey Kamugisha akipata kura 75, Gabriel Mkumbi 71, huku mtetezi Nicholas Muyuwa akila 5.

Bwilingu diwani wa zamani Ahmed Nassar amerejea kwa kura 122 akimshinda aliyetetea Lucas Lufunga kura 82, huku kiongozi mkongwe Mbwana Madeni akiondoka na kura 18.

Kata ya Talawanda Ramadhani Biga 83 akimpita Sephu Mbeyu 63 kata ambayo mtetezi wake Said Zikatimu alijitosa Ubunge ambapo kura hazikutosha, Kata ya Pera Jackson Mkango kura 47 dhidi ya Shukuru Mbato 43, na Hussein Mramba 30.

Vigwaza ambapo mtetezi Mohsin Bharwan hakutetea, Mussa Gama 91, Athumani Kimui 41 akifungana na Paul Samuel Jang'andu 41, huku Miono Juma Mpwimbwi Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri akipata kura 192 dhidi ya 94 za Masoud Zando.

Kata ya Kiwangwa Malota Kwaga akimshinda Rehema Mno kwa kura 169 dhidi ya 15 za mpinzani wake, huku Rehema Mwene akiendelea kung'ang'ania Kata ya Lugoba kwa kura 92 dhidi ya Karama Ahmed Tamimu 75.
Mpya zaidi Nzee zaidi