Merkel ameongeza kuwa Ujerumani itahimiza kuwepo makubaliano wakati wa mkutano wa kilele wa nchi hizo kati ya tarehe 17 hadi 18 wiki hii. Merkel amesema hakuna uhakikisho kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya watakubaliana kuhusu pendekezo la rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel, linalolenga kuusaidia umoja huo kukabiliana na hali mbaya zaidi ya uchumi tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kufuatia janga la corona.
Merkel aliyasema hayo jana baada ya mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez. Michel amewasilisha bajeti ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya ya euro trilioni 1.074, pamoja na mfuko wa euro bilioni 750, kusaidia uchumi ambao umeathiriwa na janga la corona.
