Rais wa Uturuki azungumza na Donald Trump kwa njia ya simu


Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan azungumza kwa njia ya simu na rais wa Marekani Donald Trump.

Katika mazungumzo yoa viongozi hao wawili wamejadili kuhusu  ushirikiano katikasekta ya biashara na kiwango cha dola bilioni  100.

Vile vile katika  mazungumzo yao viongozi hao wawili wamezungumza kuhusu ushirikiano kati ya mataifa yao hayo mawili katika nyanja tofauti.

Kuhusu hali inayoendelea nchini Libya,  viongozi wa mataifa hayo mawili wameafikiana  kuendelea na ushirikiano katika kutafuta suluhu kunako mzozo wa Libya.