Chama cha Wananchi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kinawasihi wazazi wachukuwe tahadhari juu ya malezi ya watoto wao na waache kutumia adhabu nzito au za kidhalilishaji wakati kuwapa adabu.
TAMWA ZNZ inaeleza hayo kufuatia tukio lililotokea hivi karibuni huko Bububu Kihinani kilichomshirikisha, Bi Asma Said, na msichana wake wa kike kwa kumvua nguo, na kumtupa nje akiwa hana nguo.
Tukio hilo ni kama ukatili wa majumbani, suala la jinsia, haki za binadamu na pia ni kinyume cha sheria kwa hivyo wazazi wanapaswa kujitahidi kutokutenda makosa haya yasiyostahili na kuwaweka watoto katika hali hii ya udhalilishaji.
TAMWA pia inawaomba wazazi kuelewa kuwa hatua ya ujana, ya wasichana na wavulana inahitaji uvumilivu zaidi na ushauri kutoka kwa watu mbali mbali hususan wazazi / walezi.
Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari ambayo ilirushwa na redio ya ZBC mnamo Julai 21, 2020, maarufu kama kipindi cha mawio, mlezi huyo alikasirishwa na kitendo cha msichana huyo kuingia ndani ya chumba chake (cha mlezi) na kutumia vipodozi / mafuta yake ya mwili.
Kwa hivyo TAMWA Zanzibar ingependa kuwakumbusha wazazi kwamba vitendo vya unyanyasaji kwa watoto havikubaliki kwani vinawaathiri watoto/wasichana kimwili, kiakili na kisaikolojia.
Msichana mwenye umri wa miaka 14 ni mtoto mkubwa sana na kuvuliwa nguo zake haipaswi kuwa ni adabu bora kwake.
Katika suala hili, kwa hivyo, TAMWA Zanzibar inapenda kuwaomba wazazi kushughulikia kwa uangalifu mabadiliko ya tabia ya watoto katika hatua ya mpito ya utoto kuelekea ujana ili kuwaongoza na kuepuka mzozo usio wa lazima.
Hichi ni kipindi kigumu kwao katika maisha yao kwa vile wanapata mabadiliko mapya katika miili yao na wakati mwengine hushindwa kukabiliana nayo vizuri.
Tunatoa wito pia kwa vyombo vinavyotekeleza sheria kulipa uzito suala hilo kwa kutoa adhabu inayofaa.
